Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo wake mpya ‘Cash Madame’, ameandika kwenye mtandao wa Instagram kuwa siku za kipindi cha kumtegemea mwanaume kwa sasa kimepitwa na wakati.
Kupitia mtanda huo, Vanessa ameandika:
Wimbo huu ni tamko langu kwa wanadada zangu wanaojitegemea. Siku za kumtegemea mwanaume kwa namna yeyote ile zimepitwa na wakati. Afrika mpya inabidi ihamasishe wanawake wawe na mawazo huru ya kutomtegemea mwanaume. Nikiwa binti kama huyo, nimeangaliwa tofauti mara kadhaa, ila #CashMadame bila kuzingatia kazi yake wala mfuko wake, hatetereshwi na ana uhuru mkubwa!
0 comments:
Post a Comment