Timu ya Arsenal imemaliza Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi kwa kuwa ya kwanza katika kundi A, baada ya kuifunga Basel magoli 4-1 huku magoli matatu yakifungwa na Lucas Perez.
Ushindi huo umeifanya Arsenal kuipiku Paris St-Germain iliyotoka sare ya magoli 2-2 dhidi ya Ludogorets Razgrad, katika mchezo ambao ambao walikuwa wanahitaji ushindi wa aina yoyote ule ili kuongoza kundi hilo.
Lucas Perez alifunga goli la kwanza katika dakika ya nane na kuongeza la pili dakika ya 16 kabla ya kuhitimisha hat-trick yake katika dakika ya 57. Alex Iwobi alifunga goli la nne kabla ya Seydou Doumbia kufunga goli pekee la Basel.
Lucas Perez akifunga goli lake la pili katika mchezo huo
Katika mchezo mwingine Manchester City ambayo imeshajihakikisha kutinga hatua ya mtoano katika ligi ya Mabingwa Ulaya ilijikuta ikilazimika kuchomoa goli na kutoka sare ya 1-1 na Celtic katika dimba la Etihad Stadium.
Celtic ilipata goli lake kupitia mchezaji anayecheza kwa mkopo winga Patrick Roberts katika dakika ya nne tu ya mchezo kwa kumalizia vizuri pasi aliyopewa, lakini furaha yao ilidumu kwa dakika nane tu kabla ya Kelechi Iheanacho kusawazisha.
Patrick Roberts akiwa amemzidi maarifa kipa Willy Caballero
0 comments:
Post a Comment