NAY WA MITEGO-: NYUMBA YA DIAMOND YA SOUTH MIMI NIMEIJENGA TABATA



Jana kwenye XXL ya Clouds FM Nay wa Mitego alikuwepo kutambulisha ngoma yake mpya ambayo ameipa jina la Sijiwezi...
Ndipo alipokutana na story ya list ya wasanii 10 wa Bongo Fleva ambao wamefanikiwa kumaliza ujenzi wa nyumba zao na ikiwa mtonyo wa kijenga nyumba hizo umetokana na music.
Diamond Platnumz alikuwa ni mmoja kati ya wasanii waliopo kwenye list hiyo ambaye yeye inasemekana amenunua nyumba yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Million 300 huko nchini South Afrika.
Ndipo Nay wa Mitego alipoikamatia hiyo kwa juu na kudai kuwa mjengo ambao Diamond Platnumz ameujenga South Africa, yeye ameujenga hapa hapa Bongo pande za Tabata. Akiwa na maana kuwa nyumba yake ambayo ameijenga Tabata ina thamani sawa na nyumba ya Diamond Platnumz ya huko South Africa (Mil 300).
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment