Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, ametoa muda wa mwezi mmoja kwa uongozi wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam kuhakiki mali zake kabla ya kuanza zoezi la ukaguzi wa mali hizo.
Kinana alitoa agizo hilo wakati akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa jengo la CCM tawi la Kibasila. Alitoa onyo kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia mali ya chama hicho kinyume na taratibu zilizowekwa na kukwamisha mikakati ya chama hicho kujijenga.
“Natoa mwezi mmoja kwa mkoa wa Dar es Salaam, kujiridhisha na uhakiki huo wa mali baada ya hapo baada ya mwezi mmoja nitafanya ziara ya mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Kinana.
BY: EMMY MWAIPOPO
0 comments:
Post a Comment