Kabla hawajacheza mchezo dhidi Man City kocha wa Arsenal Arsene Wenger ametoa taarifa kuhusu majeruhi ya Danny Welbeck ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha lake la goti, Welbeck anatarajiwa kuungana na timu baada ya siku 7 hadi 10 zijazo.
Hivyo hiyo ni good news kwa mashabiki wa Arsenal kuhusu mchezaji huyo aliyekuwa akiuguza jeraha lake la goti toka mwezi May na ilitarajiwa kuwa inawezekana akawa nje ya uwanja kwa miezi 9, ila Wenger amethibitisha nyota huyo kuendelea vizuri na ataungana na wachezaji wenzake hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment