Mtoto wa Rais wa zamani wa Msumbiji ameuwawa na mume wake


Mtoto wa Rais wa zamani wa Msumbiji Valentina Guebuza ameuwa mjini Maputo Msumbiji alfajiri ya leo December 15 2016 kwa kupigwa risasi na mume wake.
Valentina ambaye alifariki akiwa anakimbizwa hospitali ameuwa kwa kupigwa risasi nne na mumewe, msemaji wa Polisi Msumbiji Orlando Mudumane amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa mume wa Valentina amekiri kufanya mauaji.
Mume wa Valentina amekiri kufanya mauaji hayo baada ya kuwa na migogoro na mkewe katika ndoa yao, Valentina ambaye alikuwa anatajwa kuwa miongoni mwa wanawake matajiri Afrika, alikuwa ni mtoto wa Rais wa zamani wa Msumbiji Armando Emilio Guebuza.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment