Lionel Messi amekutana na mtoto wa kiume raia wa Afghanistan ambaye alitengeneza mfuko wa plastiki kama fulana ulioandikwa Messi 10.
Messi amekutana na mtoto huyo Murtaza Ahmadi, jana katika mchezo wa kirafiki na Al-Ahli ambao Barcelona ilishinda kwa magoli 5-3, nchini Qatar.
Katika mchezo huo Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wote walitikisa nyavu wakati Barcelona ikiifunga Al-Ahli huko Qatar.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka sita alipata umaarufu baada ya picha yake kuwekwa kwenye mitandao ya jamii akiwa na jezi hiyo ya nyota wake ampendaye.
Dogo akiwa amepozi na jezi yake ya Lionel Messi aliyoitengeneza kwa kutumia mfuko wa plastiki
0 comments:
Post a Comment