Adam Lallana ametupia magoli mawili na kutengeneza nafasi ya goli la tatu na kusaidia kuipatia Liverpool ushindi wa ugenini wa magoli 3-0 dhidi ya Middlesbrough.
Liverpool ilishuka katika dimba la Riverside ikiwa imefanikiwa kuambulia pointi moja tu katika michezo yake miwili iliyopita na kocha Jurgen Klopp alimuweka benchi kipa Loris Karius.
Katika mchezo huo Sadio Mane alipoteza nafasi kadhaa lakini Lallana hakufanya makosa na umahiri wake uliipatia Liverpool goli la tatu lililofungwa na Divock Origi.
Adam Lallana akifunga goli katika mchezo huo jana
Divock Origi akishangilia kwa kunyoosha mkono baada ya kufunga goli
0 comments:
Post a Comment