Wanawake 10 mastaa waliolipwa pesa nyingi zaidi kwenye muziki


Jarida maarufu la Forbes linalohusika na kuchapisha taarifa za watu maarufu duniani na rekodi mbalimbali leo November 3, 2016 limetaja list ya mastaa wa kike kwenye muziki wanaolipwa pesa nyingi zaidi mwaka 2016.
Mwimbaji wa muziki wa Country Taylor Swift ameongoza kwenye orodha hiyo kwa kuingiza dola za Marekani Milioni 170, akimpita mara mbili Adele aliyeshika nafasi ya pili.
Kwa mujibu wa Forbes, mapato mengi aliyopata Taylor Swift mwenye umri wa miaka 26 yametokana na ziara yake iitwayo 1989 ambayo imetajwa kumuingizaia dola za Marekani Milioni 250 huku ziara ya North America pekee ikitajwa kumuingizia dola za Marekani Milioni 200.
Full list ndio hii hapa chini:
1. Taylor Swift (Dola Milioni 170)
2. Adele (Dola Milioni 80.5)
3. Madonna (Dola Milioni 76.5)
4. Rihanna (Dola Milioni 75)
5. Beyoncé (Dola Milioni 54)
6. Katy Perry (Dola Milioni 41)
7. Jennifer Lopez (Dola Milioni 39.5)
8. Britney Spears (Dola Milioni 30.5)
9. Shania Twain (Dola Milioni 27.5)
10. Celine Dion (Dola Milioni 27)
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment