TIMU YA MANCHESTER CITY YALIPA KISASI KWA BARCELONA


Manchester City imepambana kiume na kulipa kisasi cha kufungwa na Barcelona katika mchezo wa awali, baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 kwenye dimba la Etihad katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo huo Lionel Messi alifunga kiufundi goli lake la 90 katika ligi hiyo akimalizia pasi nzuri ya Neymar, hata hivyo goli hilo lilisawazishwa na Ilkay Gundogan akiunganisha pande la Raheem Sterling.

Manchester City ambao walikuwa wakitafuta ushindi wao wa kwanza dhidi ya Barcelona, waliandika goli la pili kupitia kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Kevin de Bruyne na kisha Gundogan kuongeza la tatu.
                              Kevin de Bruyne akipiga mpira wa adhabu ulioandika goli la pili 
    Ilkay Gundogan akifunga goli katika usiku ambao alijikuta akipachika magoli mawili
                        Lionel Messi akishangilia goli lake akiwa na Luis Suarez na Neymar
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment