Real Madrid itabidi wagojee kuweza kujihakikishia kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kutoka sare ya magoli 3-3 na Legia Warsaw, katika mchezo uliochezwa bila mashabiki.
Mchezo huo ulichezwa bila kuhudhuriwa na mashabiki kutokana na kutokea ghasia za mashabiki katika mchezo uliopita wakati Legia ilipolala 6-0 dhidi ya Borussia Dortmund na kutozwa faini ya paundi 69,000.
Katika mchezo huo Gareth Bale aliweka rekodi ya kufunga goli la mapema kabisa kwenye ligi hiyo, alilolifunga katika sekunde ya 57 tu ya mchezo na kisha baadaye kumsaidia Karim Benzema kuongeza la pili.
Legia Warsaw ilizawazisha kupitia kwa Vadis Odjidja-Ofoe na Miroslav Radovic na kisha kuongeza goli la tatu lililofungwa na Thibault Moulin strike, hata hivyo Real Madrid ilisawazisha dakika mbili baadaye kupitia kwa Mateo Kovacic.
0 comments:
Post a Comment