Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo amejifunga Real Madrid kwa kukubali kutia saini mkataba mpya utakaomuweka kwenye klabu hiyo hadi Juni 2021.
Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ureno mwenye miaka 31, mkataba wake wa sasa unaisha Juni 2018, lakini hii leo atatia sani mkataba mpya wa miaka mitano.
Chini ya mkataba huo mpya imeripotiwa kuwa mshahara wa wiki wa Ronaldo utabakia paundi laki 365,000. Ronaldo ameifungia Real Madrid magoli 371 tangu ajiunge nayo mwaka 2009.
Cristiano Ronaldo akiwa amepozi na kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Real Madrid kulitwaa
0 comments:
Post a Comment