Timu ya Manchester United imemaliza ukame wa kutokushinda michezo minne ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuifunga Swansea City kwa magoli 3-1.
Manchester United iliutawala mchezo huo tangu mwanzoni na kufanikiwa kufunga magoli 3-0 hadi mapumziko, Paul Pogba akifunga goli la shuti kali huku Zlatan Ibrahimovic akitupia mawili.
Mike van der Hoorn aliifungia goli Swansea kipindi cha pili huku wageni Manchester United wakionekana kutotishiwa na safu ya Swansea, katika mchezo huo ambao kocha Jose Mourinho aliushuhudia akiwa jukwaani baada ya kufungiwa.
Zlatan Ibrahimovic akiachia shuti lililoza goli lake la kwanza hapo jana
Zlatan Ibrahimovic akishangilia goli lake kwa kuruka teke la kung fu
0 comments:
Post a Comment