Gareth Bale amesherehekea mkataba wake mpya kwa kufunga magoli mawili katika ligi ya La Liga na kuisaidia vinara Real Madrid kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Leganes.
Katika mchezo huo Real Madrid walionekana kutofanya vyema hadi pale Gareth Bale alipofunga goli la kwanza akiunganisha pande la Isco, kisha kuongeza la pili na baadaye Alvaro Morata kufunga la tatu.
Gareth Bale akifunga goli baada ya kumzidi golikipa maarifa
Cristiano Ronaldo akiachia shuti ambalo halikulenga shabaha golini
Katika mchezo mwingine wa La Liga Luis Suarez ameihakikishia Barcelona ushindi baada ya kufunga goli la pili katika kipindi cha pili na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Sevilla. Katika mchezo huo Vitolo aliifungia Sevilla goli la kwanza lililosawazishwa na Lionel Mess.
0 comments:
Post a Comment