Rais wa Real Madrid Florentino Perez na meya wa jiji la Madrid Manuela Carmena wameweka hadharani project hiyo sambamba na michoro ya uwanja huo utakavyokuwa, mradi huo ambao utakamilika katika kipindi cha miaka mitatu unatajwa kuwa moja kati ya kivutio cha mji wa Madrid hususani nyakati za usiku kwa aina za taa zitakazowekwa.
Perez amesema ukarabati wa uwanja huo hautahusisha ongezeko la watu wanaoingia uwanjani, bali idadi ya watu wataendelea kuwa 81000 kama kawaida, isipokuwa viti 3000 vitabadilishwa katika uwanja huo, ukarabati huo utagharimu zaidi ya pound milioni 360 ambazo ni zaidi ya bilioni 950 za kitanzania.
0 comments:
Post a Comment