Man United bado hali ngumu, walazimishwa sare Old Trafford na vibonde


Bado mambo sio mazuri kwa upande wa kocha wa Man United na vijana wake Jose Mourinho, kutokana na leo October 2 2016 kushuka tena katika uwanja wake wa Old Trafford kucheza mchezo wa 7 wa Ligi Kuu England dhidi ya Stoke City.

3905e66200000578-3818183-image-a-21_1475412141980
Man United ambao wengi walikuwa wanawatazamia kuwa wataondoka na ushindi dhidi ya Stoke City kutokana na kucheza nyumbani na Stoke City kuwa vibonde katika Ligi Kuu England msimu huu, wamelazimishwa sare ya kufungana goli 1-1.
3905e30700000578-3818183-image-a-46_1475412984578
Licha ya Man United kuutawala mchezo kwa asilimia 67 kwa 33, waliitumia nafasi moja tu dakika ya 69 kupitia Anthony Martial na kuandika goli la kwanza, goli ambalo Stoke City walisawazisha dakika 8 kabla ya mchezo kuisha kupitia kwa Joe Allen.
asa
Msimamo wa EPL baada ya mechi ya Man United vs Stoke City
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment