Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezifungia rasmi timu za Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka pale zitakaporuhusiwa tena na Serikali.
Nape ametoa amri hiyo leo Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung'oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo.
"Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu," alisema Nape.

0 comments:
Post a Comment