Inaweza ikawa mara ya kwanza kusikia neno”Socialite”,au pengine umeshawahi kusikia mtu akizielezea sifa za mtu kwa kumuita “Socialite person”,ila kwa kifupi “Socialite” ni neno la kingereza linalomwelezea mtu mwenye sifa nyingi ila baadhi ya sifa hizo ni pamoja na kuzungumziwa kwenye vyombo habari mara kwa mara,nguvu ya fedha,kuonekana kwenye matamasha na event mbalimbali za burudani,kujihusisha na masuala ya kijamii ect.
Kwa kuzingatia sifa hizo hii hapa ni top ten socialite girls wanazungumziwa na kuandamwa zaidi na vyombo vya habari Afrika mashariki.
10.HAMISA MABETO.
Mrembo huyu ni mwanamitindo aliejipatia umaarufu kwa muda mfupi kwa kuonekana kwenye video kadhaa za mastaa wa bongo fleva kama “Your Mine” ya mwanamuziki Quick Racka na kupelekea watu wengi hasa magazeti ya udaku kumfatilia.
09.GIGY MONEY.
Gigiy Money amejipatia umaarufu kwa miezi ya karibuni kwani licha kupiga picha zanazoonyesha maungo yake,ameonekana kwenye video nyingi za bongo fleva,baadhi ya video hizo ni “I get high” ya rapper Godzila, na”Shika adabu yako”ya Ney wa mitego,mbali kuonekana kwenye video hizo Gigy money ametajwa mara kadhaa kwenye headline za magazeti ya udaku akidaiwa kutoka kimapenzi na baadhi ya mastaa wa muziki.
08.VANESSA CHITTLE.
Mrembo huyu ambae pia ana kipaji cha muziki,amekua akihost shows mbalimbali jijini Nairobi.Baada ya picha zake za utupu kuvuja kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya alipata umaarufu na kufanya watu wengi hasa magazeti ya udaku kuanza kumfatilia.
07.RISPER FAITH.
Mrembo huyu mwenye shepu matata,amekua kwenye headline za magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii nchini Kenya kwa skendo za kutoka kimapenzi na watu maarufu,mbali na skendo hizo Risper amekua akidai kuwa yeye ni mkirsto na anaamini Yesu ameokoa maisha yake.
06.JUDITH HEARD.
Mbali na kuonekana kwenye video ya Jose Chamilion inayofahamika kama “Vumilia”,mrembo huyu kutoka Uganda ni mwanamitindo wa kimataifa na mjasiriamali ambae amekua kwenye headline za vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini Uganda akidaiwa kutoka kimapenzi na vijana aliowazidi umri.
05.VERA SIDIKA.
Mrembo huyu alijipatia umaarufu mara baada ya kuonekana kwenye video inayofahamika kama”You Guy”ya kundi la muziki la P-Unit iliyotoka mwaka 2012,mbali na video hiyo pia alionekana kwenye video inayofahamika kama “Carry Go” ya Nigerian musician Davido aliyomshirikisha D-Black,licha ya kutokea kwenye video hizo Queen V kama anavyojiita ameonekana kwenye season one ya reality show inayofahamika kama “Nairobi Diaries”.
04.HUDDAH MONROE.
Mrembo huyu kutoka Kenya alijipatia umaarufu zaidi mwaka 2015 aliposhiriki kwenye shindano la “Big Brother Africa”,ingawa hakushinda ila Huddah ameendelea kubaki kwenye headline za media houses,magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii akiwa na skendo za kutoka kimapenzi na watu maarufu na mastaa wa muziki nchini Kenya.
03.AGNESS MASOGANGE.
Mrembo huyu mwenye shepu inayowatoa wanaume udenda,ameonekana kwenye video kadhaa za bongo fleva kama “Masogange” ya Belle 9 ambayo ilimpatia jina analolitumia mpaka leo,pia alionekana kwenye video inayofahamika kama “Msambinugwa” ya Tunda man f.t Ally Kiba.mbali na kuonekana mara kadhaa kwenye events za burudani,mrembo huyu aliingia kwenye headline za media houses Tanzania na nnje ya nchi mwaka 2013,alipokamatwa na polisi nchini Afrika Kusini akidaiwa kusafirisha kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya aina ya “Crystal methamphetamine”,Agness pia amewahi kuandikwa mara kadhaa kwenye headline za magazeti ya udaku Tanzania akidaiwa kutoka kimapenzi na mastaa wa muziki akiwemo Nigeria musician,Davido.
02.ZARI HASSAN.
Mrembo huyu licha ya kuwa mama wa watoto wanne,watatu wa kiume na wa kike “Princess Tiffa”aliezaa na Mogul Bongofleva star,Diamond Platnumz,ni mfanyabiashara anaemiliki magari kadhaa ya kifahari na nyumba katika nchi za Uganda na Afrika kusini,mahusiano yake na Diamond yamezidi kumfanya afatiliwe na kuzungumziwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
01.CORAZON HASSAN.
Mrembo huyu msomi aliehitimu masomo ya sheria katika chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya,ni mwanamitindo aliejipatia umaarufu mara baada ya picha zake za utupu kuvuja kwenye mitandao ya kijamii,kama ilivyo kwa warembo wenzake Carazon amewahi kutokea kwenye kurasa za mbele za magazeti ya udaku nchini Kenya akihusishwa na za kutoka kimapenzi na watu maarufu na mastaa wa muziki nchini Kenya na kumfanya azidi kuandamwa na mapaparazi kila kukicha.
0 comments:
Post a Comment