TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WA DAR ES SALAAM WANAOPATA UMEME KUTOKA VITUO VYA KUNDUCHI NA MAKUMBUSHO-KINONDONI KASIKAZINI


SHIRIKA la Umeme Tanzania ( TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa leo Jumamosi tarehe 24/09/2016 kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza Umeme cha Ubungo 220kV/ 132kV na kusababisha kukosekana Umeme kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam yanayotegemea Vituo vya Kumduchi na Makumbusho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu jijini mapema leo, tayari hatua za kurekebisha hitilafu hiyo zinaendelea kuchukuliwa ambapo mafundi wa TANESCO wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo na umeme utarejea masaa machache yajayo.

Taarifa hiyo inawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu wowote utakaojitokeza.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment