Goli la kipindi cha pili la Neymar
limeipatia Brazil ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Colombia na kuifanya
kupata ushindi wa pili katika michezo ya kuwania kufuzu kutinga
michuano ya kombe la dunia 2018.
Wenyeji Brazil walianza vyema kwa
kupata goli baada ya sekunde 80 tu Miranda aliporuka juu na kufunga
kwa mpira wa kichwa ikiwa ni goli lake la kwanza kuifungia Brazil
katika michezo 33 aliyoichezea.
Brazil ikiwa chini ya kocha Tite,
ilikitawala kipindi cha kwanza kwa pasi safi, lakini hata hivyo
Colombia ilifanikiwa kusawazisha goli katika dakika ya 35, lakini
Neymar aliipatia Brazil goli la pili katika kipindi cha pili.
Mchezaji tegemeo wa timu ya Brazil Neymar akifanya vitu vyake
Kocha Tite akimkumbatia Neymar kumpongeza
0 comments:
Post a Comment