Mchezaji Kinda wa Manchester United
Marcus Rashford ametakata katika mchezo wa timu ya taifa ya Uingereza
chini ya umri wa miaka 21 kwa kufunga magoli matatu 'hat trick' na
kutuma ujumbe tosha kwa makocha Jose Mourinho na Sam Allardyce juu ya
umuhimu wake.
Katika mchezo huo ambao Uingereza
iliibuka na ushindi mnono wa magoli 6-1 dhidi ya Norway, Rashford
alikuwa wa kwanza kuifungia Uingereza, Nathaniel Chalobah alifunga la
pili na Ruben Loftus-Chee la tatu, Rashford akafuga mawili mengine
Lewis Baker akafunga la sita.
Marcus Rashford akimchambua kipa kwa mkwaju wa penati na kufunga goli
Sio Ronaldo tu hata mimi naweza: Rashford akipiga mpira kwa madoido
Kocha wa timu ya wakubwa ya Uingereza Sam Allardyce akimpigia makofi Rashford kuonyesha kumkubali
0 comments:
Post a Comment