Leicester City wamesherehekea ushindi wao wa kwanza wakicheza mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata ushindi wa kishindo wa magoli 3-0 dhidi ya klabu ya Brugge, ya Ubelgiji.
Marc Albrighton aliifungia goli la kwanza Leicester City kwa shuti kufuatia makosa ya beki wa kulia Luis Hernandez, na kisha baadaye Riyad Mahrez alifunga la pili kwa mpira wa adhabu alioupiga kwa kuzungusha.
Alikuwa Riyad Mahrez aliyepachika tena goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya mshambuliaji Jamie Vardy kuangushwa katika eneo la hatari na golikipa.
Marc Albrighton akiifungia goli la kwanza Leicester City
Riyad Mahrez akiangali mpira wake wa adhabu alioupiga ukielekea wavuni
0 comments:
Post a Comment