Baada ya michezo nane kuchezwa usiku wa Septemba 13 2016, Jumanne ya septemba 14 michezo 9 ya hatua ya makundi ya michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya ilichezwa barani Ulaya, miongoni mwa michezo iliyochezwa usiku wa Septemba 14 ni pamoja na mchezo wa Real Madrid dhidi ya Sporting CP.
Sporting CP ni klabu ilimyolea Cristiano Ronaldo kutokea academy yao, hata hivyo hiyo haikuwa mechi rahisi kwa Real Madrid kwani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 ila walilazimika kusubiri hadi dakika ya 90 kujihakikishia ushindi huo kupitia goli la kichwa la Alvaro Morata ikiwa ni dakika moja imepita toka Ronaldo asawazishe goli.
Goli la Sporting CP lilifungwa dakika ya 47 na Bruno Cesar lakini mchezo huo ulimalizika kwa Cristiano Ronaldo kuondoka uwanjani akiwa kavunja rekodi ya mkongweDel Piero, kufuatia goli la faulo alilofunga Ronaldo anakuwa kafunga jumla ya magoli 12 ya faulo katika UEFA na kuvunja rekodi ya Del Piero aliyekuwa kafunga goli 11 kwa faulo.
0 comments:
Post a Comment