Sergio Aguero ametupia wavuni magoli matatu yaani hat-trick ya kwanza kwa msimu huu wakati Manchester City ikiwachachafya Borussia Monchengladbach kwa magoli 4-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo wa kwanza kwa Pep Guardiola katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Manchester City, Aguero aliunganisha krosi ya Aleksandar Kolarov na kuandika goli la kwanza na kisha kuongeza la pili kwa penati baada ya Ilkay Gundogan kuchezewa rafu.
Kama hiyo haitoshi Aguero alipachika goli lake la tatu mbele ya mashabiki 32,000, katika mchezo huo ambao ulihairishwa kufanyika jumanne kutokana na mvua kubwa. Kelechi Iheanacho akitokea benchi alifunga goli la nne kwa shuti la umbali wa yadi 12.
Sergio Aguero akielekea kufunga goli lake la tatu na kukamilisha hat-trick
Kelechi Iheanacho akifunga goli la nne la Manchester City
0 comments:
Post a Comment