RIO 2016: NEYMAR AISAIDIA BRAZIL KUTINGA NUSU FAINALI


Neymar amefunga goli lake la kwanza wakati wenyeji wa michuano Olimpiki timu ya Brazil wakiwafunga Colombia kwa magoli 2-0 na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo kwa mchezo wa soka.

Mshambuliaji huyo wa timu ya Barcelona alipiga mpira wa adhabu wa kuzungusha na kupachika goli katika dakika ya 12, na kisha Luan aliongeza la pili katika kipindi cha pili kwa shuti zuri la kunyanyua mpira juu uliojaa wavuni.

Kwa ushindi huo Brazil sasa watacheza na Honduras katika mchezo wa nusu fainali, baada ya Honduras kuifunga Korea Kusini goli moja kwa bila lililopachikwa na Albert Elias. Ujerumani itaavaana na Nigeria.
                 Mpira uliopigwa na Luan ukijaa wavuni na kuandika goli la pili la Brazil
   Refa akimpatia kadi ya njano Neymar baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Colombia
Mchezo huo uligubikwa na matukio ya wachezaji kutishiana kuonyeshaba ubabe kama inavyoonekana hapa
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment