MO FARAH ASHINDA MBIO ZA MITA 10,000 NA KUWEKA REKODI UINGEREZA


Mwanariadha wa Uingereza Mo Farah mwenye asili ya Somalia amefanikiwa kutetea ubingwa wa mbio za mita 10,000 katika michuano ya Olimpiki na kutwaa medali ya dhahabu.

Katika mbio hizo Farah alijikuta akianguka katika raundi ya 10 baada ya kukwatuliwa kwa bahati mbaya na mwanariadha mwenzake Galen Rupp, lakini alinyanyuka na kuendelea.

Mwanariadha wa Kenya Paul Tanui alipambana vilivyo na kumpita Farah, lakini bingwa huyo alizidisha kasi na kumpita. Farah anakuwa Muingereza wa kwanza kushinda medali tatu za dhahabu za Olimpiki.
   Mo Farah akishangilia ushindi baada ya kufanikiwa kuibuka mbabe wa mbio za mita 10,000
                Mo Farah akiwa amepiga magoti na kumshukuru Mungu kwa ushind
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment