Imamu na msaidizi wake wameuwawa kwa kupigwa risasi wakitembea mtaani wakati wakitoka msikiti Jijini New York nchini Marekani.
Msemaji wa polisi amesema wawili hao walifuatiliwa kwa nyuma na mwanaume mmoja aliyewapiga risasi vichwani.
Imamu Maulama Akonjee, 55, alihamia mji huo akitokea Bangladesh miaka miwili iliyopita kwa mujibu wa ripoti za Jijini New York.
Polisi wamesema kuwa hakuna ripoti zinazoashiria kuwa Imamu huyo na msaidizi wake walishambuliwa kutokana na imani yao.
Waumini wakiwa wamepigwa na butwaa baada ya kupata taarifa za kifo cha Imamu wao na msaidizi wake
Waumini wakipaza sauti zao kutaka haki itendeke kufuatia vifo hivyo
0 comments:
Post a Comment