KOCHA WA KENYA ALIYEJIFANYA KUWA MWANARIADHA RIO NA KUFANYIWA VIPIMO AREJESHWA NYUMBANI


Kocha ya wanamichezo wa riadha wa Kenya waliopo Rio nchini Brazil amerudishwa nyumbani baada ya kujifanya ni mwanariadha na kutoa sampuli ya haja ndogo kwa ajili ya vipimo.

Kenya imesema kocha huyo John Anzrah alijifanya ni mwanariadha wa mbio za mita 800 Ferguson Rotich na kutia saini nyaraka za vipimo vya kubaini matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku.

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Olimpiki Kip Keino amesema kuwa kamati yake haiwezi kuvumilia kitendo hicho alichokifanya kocha huyo.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment