Nyota wa filamu wa Bollywood, Shah Ruh Khan, ametumia akaunti yake ya twitta kuonyesha kukerwa na kitendo cha kushikiliwa kwa muda na mamlaka za Marekani katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Los Angeles.
Haikufahamika mara moja kwanini Khan alishikiliwa katika uwanja huo wa ndege wa Marekani na ni kwa muda gani.
Mwaka 2012, Wahindi walichukizwa baada ya Khan kushikiliwa kwa dakika 90 katika uwanja wa White Plains karibu na Jiji la New York.
0 comments:
Post a Comment