DIEGO COSTA, OSCAR, EDEN HAZARD NA PEDRO WAIZAMISHA WERDER BREMEN


Magoli yaliyofungwa na Diego Costa, Oscar, Eden Hazard na Pedro yameipatia Chelsea ushindi katika mechi ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Werder Bremen ya Ujerumani, hata hivyo kocha Antonio Conte bado anashida ya ukuta wa timu yake.

Katika mchezo huo Chelsea ilipata magoli mawili ndani ya dakika 10 za mwanzo wa mchezo huo kupitia kwa Hazard na Oscar na kuwafanya waongoze kabla ya Claudio Pizarro kuchomoa goli moja kwa mkwaju wa penati.

Katika kipindi cha pili Diego Costa aliifungia Chelsea goli la tatu na baadaye mchezaji wa Werder Bremen, Lennart Thy alifunga goli la pili, lakini mambo yalizidi kuwa magumu pale Pedro alipofunga goli la nne katika dakika za mwisho.
                     Eden Hazard akiachia shuti lililoandika goli la kwanza kwa Chelsea
                                 Diego Costa akiachia shuti lililoandika goli la tatu la Chelsea
    N'Golo Kante akiwania mpira uliokuwa ukimilikiwa na mchezaji wa Werder Bremen
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment