Alex Iwobi, Theo Walcott pamoja na Chuba Akpom wameizamisha Manchester City kwa magoli 3-2 katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Katika mchezo huo Sergio Aguero aliifanya Manchester City iongoze manamo dakika ya 30 kwa kuachia shuti la karibu kufuatia krosi iliyopigwa na Raheem Sterling. Alex Iwobi alisawazishia Arsenal kwa shuti la kuzungusha lililomshinda kipa Joe Hart.
Alex Iwobi akiifungia Arsenal goli la kusawazisha
Sergio Aguero akiifungia Manchester City goli la kwanza
Kelechi Iheanacho akiruka juu na kupiga mpira wa kichwa ulioiandikia Manchester City goli la pili
0 comments:
Post a Comment