BILL CLINTON AMWAGIA SIFA MKEWE BI. HILLARY CLINTON


Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amemnadi mkewe Hillary mbele ya wajumbe wa Democrat kwa kumuelezea kuwa ni rafiki mzuri, anayeweza kuliongoza taifa la Marekani.

Katika hotuba yake kwenye mkutano wa kitaifa wa chama cha Democrat huko Philadelphia, amemuelezea mkewe Hillary kuwa ni mtu bora zaidi mwenye kuweza kufanya mabadiliko.

Mapema kabla ya hotuba hiyo, Bi. Hillary Clinton aliingia katika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuteuliwa na chama kikubwa kuwania urais wa Marekani.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa chama cha Democrat wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Bill Clinton
Chelsea Clinton kati kati akisimama juu pamoja na baadhi ya wajumbe kumpigia makofi baba yake Bill Clinton
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment