Rais wa Ufaransa Fancois Hollande anakutana na viongozi wa Kikristo, Kiyahudi pamoja na Buddha, baada ya kutokea mauaji ya Padri kanisani hapo jana huko Normandy.
Padri huyo Jacques Hamel aliuwawa wakati akiendesha ibada ya asubuhi kanisani kwa kuchinjwa kwa kisu na watu waliovamia kanisa hilo.
Mmoja wa washambuliaji hao amebainika kuwa ni Adel Kermiche, 19, ambaye aliwahi kufungwa jela na aliachiwa nje akiwa chini ya uangalizi wa polisi.
Shambulizi hilo limekuja siku 12 tu kupita baada ya shambulizi la Nice ambalo watu 84 waliuwawa.
Baaada ya kukutana na viongozi wa dini, rais Francois Hollande atafanya mkutano wa ulinzi na baraza la ulinzi, na kisha baadaye kukaa na baraza la mawaziri.
Padri Jacques Hamel wakati wa uhai wake kabla ya kuuwawa kikatili
Adel Kermiche mmoja wa vijana anayehusishwa na mauaji ya Padri Jacques Hamel
0 comments:
Post a Comment