Producer Mswaki anayefahamika zaidi kwa kutayarisha ngoma mbili za Ben Pol ‘Sophia’ na ‘Ningefanyaje’, amedai ameamua kuingia rasmi kwenye muziki na kwamba amepumzika kutayarisha nyimbo za wasanii wengine.
Mswaki ambaye ni rapper tayari ameachia ngoma yake mpya iitwayo Kilele aliyomshirikisha Mwasiti.
“Ndio nimeingia rasmi kama rapper na hii ndio nyimbo yangu ya kwanza official kabisa na ambayo nairelease kwenye redio na nini,” Mswaki ameiambia Bongo5.
Mswaki amesema amewahi kutoka nyimbo kadhaa kabla lakini hazikuwa rasmi na alikuwa akizitoa mtandaoni peke yake.
0 comments:
Post a Comment