Fainali za shindano la Airtel Trace Music Star zitafanyika Jumamosi, June 11 jijini Lagos Nigeria.
Tayari majaji wa fainali hizi wametangazwa akiwemo mentor wa mwaka huu, Keri Hilson kutoka Marekani. Wengine ni Makamu Mkuu wa Rais wa Roc Nation, Shawn ‘Pecas’ Costner na msanii wa DR Congo, Fally Ipupa.
Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na Melisa John.
Mshindi wa mwaka huu kutoka Tanzania, Melisa John akikabidhiwa bendera kuiwakilisha nchi
Washiriki wengine wanatoka Ghana, Nigeria, Gabon, Malawi, DRC, Zambia, Niger na Madagascar. Mshindi wa mwaka huu atapata zawadi, kulipiwa video ya muziki, record deal pamoja na kufanya kazi Keri Hilson.
Mwaka jana muimbaji wa Tanzania, Mayunga aliibuka mshindi.
0 comments:
Post a Comment