Msanii Peter Msechu amefunguka na kusema kuwa yeye mwili wake umemshinda sasa maana amejaribu kila mbinu kupunguza lakini wapi upo pale pale na yeye mambo ya kusema afanye diet hawezi kwani hela ya kununu matunda ya elfu nne kila siku hana.
Peter Msechu amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kusema sasa amegundua kitu pekee kinachoweza kupunguza mwili wake si kufanya diet bali ni kupata stress tu, hivyo anatafuta mtu wa kumpa stress ili apungue.
"Mambo ya kusema nafanya diet mimi siwezi hizo hela za kununua matunda ya elfu nne kila siku mimi sina, sijui hela ya gym hamna, saizi mimi nataka stress tu ili nipungue maana kitambi hiki saizi kimekuwa na mazalia kama arobaini hivi" alisema Peter Msechu
Mbali na hilo Peter Msechu alisema kuwa katika wimbo wao mpya ambao wamefanya na Banana Zoro kwa asilimia kubwa umeandaliwa na Banana Zoro na kusema yeye yupo karibu na Banana Zoro kutokana na ukweli kwamba wanafanya muziki wa aina moja wa live, na kusema huo ndiyo muziki wa kweli na si muziki wa wasanii wengi wa bongo ambao wanabebwa bebwa na computer kwa kutengenezwa.

0 comments:
Post a Comment