Waandamanaji wanapanga kutumia panya 200 katika maandamano katika mji wa Nyeri mkoa wa kati nchini Kenya kulingana na gazeti la the Star nchini humo.
Gazeti hilo limemnukuu mshirikishi wa maandamano hayo John Wamagata akisema ''tutaleta panya 200 na kuwatembeza katikati ya mji''.
Gazeti hilo linaongezea kwamba maandamano hayo yanayopangwa kufanyika wiki ijayo yanapinga mapendekezo ya bunge la kaunti hiyo kutumia shilingi milioni 75 kujenga klabu ya kuimarisha afya.
Klabu hiyo itakuwa na eneo la kunyosha misuli,eneo la kuoga kwa kutumia mvuke,eneo la masaji,kidimbwi cha kuogelea na sauna kulingana na gazeti la the star.
0 comments:
Post a Comment