Gavana wa Jiji la Tokyo amesema anajiuzulu baada ya kukabiliwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Gavana Yoichi Masuzoe amekuwa akikosolewa mno kwa tuhuma za kutumia fedha za umma kwenda kutumbua mapumzikoni, na kununua kazi za sanaa na vitabu vya watoto wake.
Gavana Masuzoe anatarajiwa kupoteza katika kura ya kutokuwa na imani naye katika baraza la Jiji hilo kuu la Japan baadaye hii leo.
Ziara za Gavana Masuzoe Jijini London na Paris pia zinadaiwa kutumia fedha za umma
0 comments:
Post a Comment