Timu ya taifa ya Hungary imewashangaza watu katika michuano ya Euro 2016 baada ya kupata ushindi dhidi ya Austria waliobakia na wachezaji 10 katika mchezo wao wa kwanza katika michuao hiyo.
Katika mchezo huo Austria walikaribia kufunga goli la mapema mno katika michuano hiyo lakini shuti la David Alaba katika sekunde ya 28 liligonga mwamba.
Hungary waliwadhibiti vyema wapinzani wao Austria kwa kuongoza wakati Adam Szalai akiunganisha pasi ya Laszlo Kleinheiser na kupachika goli la kwanza na kisha Zoltan Stieber kufunga goli la pili baadaye.
Adam Szalai akiifungia Hungary goli la kwanza katika mchezo huo
0 comments:
Post a Comment