Serena Williams amemshinda Mmarekani mwenzake, Madison Keys, kwa seti zote na kutwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Italia, ikiwa ni taji lake la kwanza tangu miezi tisa kupita bila kikombe.
Mchezaji huyo namba moja duniani katika viwango vya tenesi kwa wanawake, alimshinda Mmarekani mwenzake huyo kwa seti 7-6 (7-5) 6-3 na kutwaa ubingwa wa michuano ya Roma kwa mara ya nne tangu mwaka 2002.
Williams, 34, kwa mara ya mwisho alishinda taji kwenye michuano ya Cincinnati mwezi Agosti, tangu wakati huo amepoteza michezo ya fainali ya Marekani, Australian pamoja na ya Indian Wells.
Mambo ya Selfie: Serena Williams akijipiga selfie na kombe lake
Oops! kombe likimtereza Serena Williams na mfuniko wake kuanguka
0 comments:
Post a Comment