Kipa wa Manchester United, David de Gea, yupo tayari kuachana na klabu hiyo katika msimu wa majira ya joto iwapo kocha Louis van Gaal ataendelea kuinoa timu hiyo.
Kipa huyo raia wa Hispania anahisi kuwa na wakati mgumu chini ya kocha huyo Mdachi, licha ya kusaini mkataba wa miaka minne mwanzoni mwa msimu huu.
Chanzo ndani ya Old Trafford kimesema De Gea, ambaye anatakiwa na Real Madrid, atashinikiza ili kufanikisha uhamisho wake.
0 comments:
Post a Comment