DIEGO COSTA, JUAN MATA NA TORRES WATEMWA KIKOSI CHA HISPANIA


Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa, ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016, wakati mabingwa hao watetezi wakijiandaa kutetea kombe hilo.

Kocha Vicente del Bosque pia ameamua kuwachukua wachezaji wengine wenye majina makubwa kama mshambuliaji wa Atletico Madrid, Fernando Torres, kiungo wa Manchester United, Juan Mata na nyota wa Arsenal, Santi Cazorla.

Katika kikosi chake cha wachezaji 25 kocha huyo amewaita Cesc Fabregas, Pedro, Cesar Azpilicueta, David Silva pamoja na golikipa David de Gea ambao ni wachezaji wanaosakata soko katika Ligi kuu ya Uingereza.
                                                                 Juan Mata aliyetemwa kikosi cha taifa
                                                                        Fernando Torres katemwa naye

Kikosi Kamili ni:-

Makipa: Iker Casillas (Porto), David De Gea (Manchester United), Sergio Rico (Sevilla)
Mabeki: Jordi Alba, Gerard Pique, Marc Bartra (all Barcelona), Sergio Ramos, Dani Carvajal (Real Madrid), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Juanfran (Atletico Madrid)
Viungo: Sergio Busquets, Andres Iniesta (both Barcelona), David Silva (Manchester City), Mikel San Jose (Athletic Bilbao), Koke, Saul Niguez (both Atletico Madrid), Cesc Fabregas (Chelsea), Thiago Alcantara (Bayern Munich), Isco (Real Madrid), Bruno Soriano (Villarreal)

Washambuliaji: Pedro Rodriguez (Chelsea), Alvaro Morata (Juventus), Aritz Aduriz (Athletic Bilbao), Nolito (Celta Vigo), Lucas Vazquez (Real Madrid).
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment