Abiria ndege ya ATCL waliotakiwa kusafiri kwenda Comoro wamekwama kuondoka kwa siku sita

Abiria zaidi ya 80 waliotakiwa kusafiri na ndege ya shirika la ATCL kwenda Comoro wamekwama kusafiri baada ya Ndege ya Shirika la ATCL waliyotakiwa kusafiri nayo kuharibika.

Shirika la ATCL wamesema ndege ilipata tatizo la kiufundi na tayari spare zimeingia nchini na utengenezaji unaendelea na watawasafirisha siku ya alhamisi na ikishindikana watawasafirisha kwa ndege ya shirika lingine. Shirika hilo lina ndege moja ambayo inafanya safari zake za Dar es salaam na Comoro.
Kwenye video hii fupi hapa chini ni mmoja wa abiria aliyetakiwa kusafiri na ndege hiyo ameyazungumza haya……>>> ‘tunakaribia wiki mbili kila siku tunakuja wanatuambia nendeni mtakuja tena, mpaka leo hatujui mpaka lini tutaondoka’
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment