Wafanyakazi wa kiwanda cha Sukari Ilovo wilaya Kilosa na Kilombero wametishia kusitisha kuendelea na uzalishaji wa sukari, lengo likiwa ni kushinikiza waongezwe mshahara kwa asilimia 15 badala ya asilimia 2.2 aliyokubali kuongeza muajiri baada ya kuvutana kwa muda mrefu.
Mpango wa wafanyakazi hao umeafikiwa baada ya kukaa kikao na mwenyekiti wa wafanyakazi mashambani TPAWU Isaack Magassa na kushauriana kutokana na muajiri kuongeza mshahara kwa asilimia 2.2 tofauti na sheria ambayo inaruhusu ongezeko la mshahara kufikia hadi asilimia 25.
0 comments:
Post a Comment