WALIOMUUA MWANDISHI SOMALI NAO WAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI

Wanachama wawili wa kundi la al-Shabaab wameuwawa kwa kupigwa risasi baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya mwandishi wa habari aliyeuwawa kwa mlipuko wa bomo kwenye gari, mwaka jana nchini Somalia.

Wanachama hao Abdirisak Mohamed Barow na Hassan Nur Ali, waliokiri kuwa ni wafuasi wa kundi la al-Shabaab wakati wa kesi yao, walifungwa kwenye nguzo na kutekelezewa adhabu yao ya kifo kwa kupigwa risasi.

Watu hao wawili walitiwa hatiani kwa kumuua mwandishi Hindiyo Haji Mohamed ambaye gari lake lililipuliwa kwa bomu, kwa mujibu wa Naibu Jaji wa Mahakama Kuu ya Somalia, Abdulahi Hussein Mohamed.
                Walenga shabaha wakiwa tayari kufyatua risasi ili kutekeleza adhabu hiyo
             Miili ya wanachama wa al-Shabaab ikibebwa baada ya kuuwawa kwa risas
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment