Nigeria yaona fursa nyingi za ushirikiano wa kibiashara na China



Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesema kuna fursa nyingi za ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Nigeria ambazo Nigeria haipendi kuzipoteza.
Akiongea mjini Abuja kabla ya ziara yake nchini China, Rais Buhari amesema China na Nigeria zina fursa nyingi za ushirikiano kwenye maeneo kama kilimo, uchimbaji wa madini, uzalishaji wa umeme na ujenzi wa reli na barabara.
Rais Buhari ambaye leo anatarajiwa kuanza ziara ya siku tano hapa China, amesema China ina uwezo wa kiufundi, kifedha na uzoefu, na iko tayari kuisaidia Nigeria. Amesema serikali yake itaendelea kuheshimu mikataba iliyosainiwa na serikali iliyopita na makampuni ya China kwenye ujenzi wa reli, barabara na mabwawa ya umeme.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment