Balozi wa Urusi nchini Uturuki alivyouawa na askari ambaye hakuwa zamu


Balozi wa taifa la Urusi nchini Uturuki Andrey Karlov, ameuawa December 19 2016  kwa kupigwa risasi na mtu ambaye alikuwa nyuma yake. Imeelezwa kuwa aliyemshambulia ni afisa wa polisi ambaye hakuwa kwenye zamu wakati balozi huyo alipokuwa anatoa hotuba kwenye maonesho ya picha katika mji mkuu Ankara.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuuawa kwa balozi wa taifa lake nchini Uturuki ni uchokozi ambao lengo lake ni kuvuruga juhudi za kutafuta amani Syria. Kwa upande wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amesema kuuawa kwa balozi huyo ni shambulio dhidi ya taifa la uturuki.
Picha za video zilimuonesha mshambuliaji, akiwa amevalia suti na tai, akimfyatulia risasi balozi huyo kutoka nyuma, akisema kwa sauti ujumbe kuhusu mji wa Aleppo, Syria, mshambuliaji huyo aliuawa kwa kupigwa risais na polisi.
Taarifa zinasema muuaji ni Mevlut Mert Aydintas ’22’, ambaye alikuwa anahudumu katika kikosi cha polisi cha kupambana na fujo mjini Ankara lakini haijabainika iwapo ana uhusiano wowote na kundi lolote.
Kisa hicho kilitokea siku moja baada ya maandamano kufanyika Uturuki kupinga hatua ya Urusi kumuunga mkono Rais wa Syria Bashar al-Assad. Recep Tayyip Erdogan alizungumza na Rais Putin kwa njia ya simu, na kwenye ujumbe wa video, alisema wote wawili walikubaliana kisa hicho kilikuwa “uchokozi”.
3b86325d00000578-4048844-a_police_cordon_was_put_in_place_after_the_assassination_near_th-a-18_1482179595345
Nje ya jengo ambalo kumetokea tukio
3b85dd2600000578-4048844-the_gunman_left_in_the_background_was_seen_standing_behind_andre-a-4_1482179593286
Balozi wa Urusi nchini Uturuki Andrey Karlov,
3b85da3000000578-4048844-gunman_mevl_t_mert_altintas_22_a_member_of_the_ankara_special_fo-a-1_1482179592884
Mevlut Mert Aydintas aliyemshambulia kwa risasi balozi wa Urusi nchini Uturuki
3b85d97600000578-4048844-chilling_pledge_the_gunman_said_he_would_not_leave_the_scene_ali-m-115_1482196274665 3b85f96500000578-4048844-the_gunman_ordered_visitors_attending_the_exhibition_to_leave_th-a-3_1482179593285 3b85fbd900000578-4048844-the_killer_shouted_allahu_akbar_god_is_great_we_die_in_aleppo_yo-a-2_1482179593282 3b8605c200000578-4048844-image-a-113_1482195748515 3b86085d00000578-4048844-russia_has_branded_the_assassination_of_mr_karlov_as_a_terror_at-m-114_1482196165474 3b86677500000578-4048844-the_gunman_reportedly_fired_one_shot_into_the_air_before_taking_-a-16_1482179594793 3b86565800000578-4048844-spectators_are_evacuated_from_the_gallery_after_mr_karlov_was_sh-a-6_1482179593491
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment