Goli safi la Philippe Coutinho
liliweza kuiua Manchester United na kufuta matumaini ya kutinga hatua
ya nane bora ya Ligi ya Europa baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye
mchezo wa jana katika dimba la Old Trafford.
Kikosi cha kocha Jurgen Klopp
kilikuwa kinalinda magoli yake mawili kwa bila iliyoyapata kwenye
mchezo wa awali Anfield, lakini penati ya dakika 32 iliyopigwa na
Anthony Martial lilifufua matumaini kwa United kabla ya Countinho
kuharibu mambo.
Anthony Martial akiwa na wachezaji wenzake wakishangilia baada ya kupiga penati
Kipa De Gea na beki Blind wakiwa hoi baada ya Coutinho kufunga bao
Mshambuliaji Pierre-Emerick
Aubameyang alipachika mabao mawili na kuiondoa Tottenham katika ligi
ya Europa baada ya Borussia Dortmund kuibuka na ushindi wa mabao 2-1,
na hivyo kuwa na mtaji wa mabao 5-1 ikijumuishwa na mchezo wa awali.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa raia
wa Gabon, alikuwa azuiliki katika mchezo huo wa jana usiku na
kuonyesha kwanini klabu kubwa za Ulaya zinahaha kuinasa saini yake
ili aweze kujiunga nazo.
Pierre-Emerick
Aubameyang akiwachia shuti lililojaa wavuni
You might also like:
0 comments:
Post a Comment