Kwa
mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la The Sun, zinaeleza
kwamba Pep Guardiola amekua akitoa maelekezo hayo kwa lengo la kuanza
kukifuma na kukijenga upya kikosi cha Man City.
Pep
ametoa agizo hilo, kwa kuamini Kompany ambaye ni beki kutoka nchini
Ubelgiji, hatoweza kuhimili mipango yake kutokana na mapungufu
aliyoyaona tangu alipoanza kumfuatilia msimu huu ambapo amekuwa akiumia
mara kwa mara.
Meneja
huyo ambaye atamalizana na FC Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu,
amependekeza kusajiliwa kwa beki wa kati wa klabu ya Athletic Bilbao ya
nchini Hispania, Aymeric Laporte kama mbadala wa Kompany.

Beki
huyo ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa chini ya
umri wa miaka 21, anaaminiwa na Pep Guardiola atatosha katika mikakati
ya kupeleka heshima huko Etihad Stadium, kuanzia msimu ujao.
Wakati
agizo hilo likitoka, Kompany kwa sasa anauguza jeraha ya kiazi cha mguu
alilolipata wakati wa mchezo wa mkondo wa pili wa ligi ya mabingwa
barani Ulaya hatua ya 16 bora, dhidi ya Dynamo Kyiv.
Hata
hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 29, bado anaendelea kukumbukwa kwa
makubwa aliyowahi kuitendea Man City hadi kufikia hatua ya kutajwa
katika kikosi bora cha wachezaji wa ligi ya nchini England kwa mwaka
2011, 2012 na 2014.
Kwa msimu huu Kompany amecheza michezo 12 ya ligi, kutokana kajeraha yanyomuandama mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment