Afrika ni bara ambalo
tafiti kadhaa zinafanyika na zimeendelea kufanyika, Matokeo ya Utafiti
wa Africa Wealth umeitaja Zimbabwe kuwa ndio nchi Maskini. Inatajwa kuwa
wizi wa kura, ukosefu wa kuheshimu haki za umiliki, vurugu, kukosekana
kwa uhuru wa Habari, ni baadhi ya sababu ya Taifa hilo kuanguka na kuwa
la mwisho.
Ripoti ya tatu ya mwaka ya
Africa Wealth inasema watu wanaoishi Zimbabwe ni maskini katika bara la
Afrika kwa kuwa na wastani wa pato la mtu mmojammoja ni US dola 200
ambapo ni kiasi ambacho watumishi wa umma wanakipata.
Ripoti imeeleza kuwa
>>>’haki za umiliki ni muhimu kwa kuwezesha kujenga utajiri,
Nchini Zimbabwe wamiliki wa Biashara hawana uhakika kama biashara zao au
mali zao bado ni zao, hii inajenga hali ya woga kwa yeyote kutojitokeza
kuwekeza kwenye nchi hiyo‘
Wakati Zimbabwe ikianguka
na kuwa nchi maskini, kisiwa cha Maurtius kimepanda na kuonekana kuwa
watu wake ni matajiri kwa hadi pato la US dola 21700 kwa utajiri wa mtu
mmojammoja. Mafanikio ya Mauritius yamehusishwa na kupata haki za
umiliki ambapo imeshuhudiwa watu matajiri wakihamia huko katika muongo
uliopita.
Utafiti uliofanyika kwenye nchi 20, zote zimekuwa na ongezeko la pato kwa kipindi cha mwaka 2000 na 2015, kasoro Zimbabwe
0 comments:
Post a Comment